Waefeso 5:22-24
Waefeso 5:22-24 NENO
Ninyi wake, watiini waume zenu kama vile mnavyomtii Bwana Isa. Kwa maana mume ni kichwa cha mkewe kama vile Al-Masihi alivyo kichwa cha jumuiya ya waumini, ambayo ni mwili wake, naye Al-Masihi ni Mwokozi wake. Basi, kama vile jumuiya ya waumini wanavyomtii Al-Masihi, vivyo hivyo na wake nao imewapasa kuwatii waume zao kwa kila jambo.