Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Waefeso Utangulizi

Utangulizi
Paulo aliandika waraka huu akiwa gerezani huko Rumi ili kuwatia moyo waumini wa Asia. Waraka huu ulikuwa kama mwongozo uliokusudiwa kwa makanisa kadhaa. Zaidi ya hayo, kwenye waraka huu hakuna salamu za watu binafsi, wala hakuna matatizo maalum. Paulo alielezea kwamba kanisa lilianzishwa na Mungu, akiwaelezea mpango wa Mungu wa tangu awali wa kuwaokoa watu wake kwa njia ya Kristo kwa imani. Mpango huu ulikuwako hata kabla ya ulimwengu kuumbwa. Mwenendo wa maisha mapya upo kinyume kabisa na ule wa maisha ya kale bila Kristo.
Mwandishi
Mtume Paulo.
Kusudi
Kuwaimarisha waumini katika imani yao ya Kikristo kwa kueleza asili na kusudi la kanisa, ambalo ni mwili wa Kristo.
Mahali
Rumi.
Tarehe
Kama mwaka wa 60 B.K.
Wahusika Wakuu
Paulo, Tikiko, na waumini wa Efeso.
Wazo Kuu
Mpango wa Mungu wa milele wa kuuokoa ulimwengu ulitimizwa kwa njia ya Kristo katika mwili wake.
Mambo Muhimu
Umoja katika Kristo na maisha mapya katika Kristo (2:4-6), na umoja katika mwili wa Kristo. Pia maisha Wakristo wanayopaswa kuishi kuhusu ndoa, tabia, mwenendo, wazazi na watoto, watumishi na mabwana zao.
Mgawanyo
Mpango wa Mungu, na wokovu wa wote wamwaminio (1:1–2:22)
Siri ya Injili (3:1-21)
Maisha ya Mkristo duniani (4:1–5:21)
Jinsi Wakristo wapaswavyo kuhusiana (5:22–6:9)
Kupigana na uovu (6:10-24).

Iliyochaguliwa sasa

Waefeso Utangulizi: NEN

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia