Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Esta Utangulizi

Utangulizi
Kitabu hiki kinachukua jina la mhusika mkuu, ambaye ni Esta. Jina hili limetokana na neno la Kiajemi ambalo maana yake ni “Nyota.” Jina la Esta la Kiebrania ni “Hadassah,” maana yake “Mhadasi” ambayo ni aina ya miti iliyokuwa inastawi milimani karibu na Yerusalemu, na ilikuwa inatumika kujengea vibanda wakati wa Sikukuu ya Vibanda. Kitabu hiki kinaeleza kuhusu kisa cha msichana mzuri wa Kiyahudi ambaye Mfalme Ahasuero wa Kwanza alimchagua awe malkia wake.
Matukio yaliyowapata Wayahudi yanayoelezwa kwenye kitabu hiki yalitokea huko Shushani, uliokuwa mji mkuu wa Uajemi chini ya utawala wa Mfalme Ahasuero aliyetawala Uajemi mnamo 486–465 K.K. Kule kuokolewa kwa Wayahudi kwa ajabu wakati wa Mfalme Ahasuero baadaye kuliadhimishwa kila mwaka kama Sikukuu ya Puri. Wakati huu, kitabu cha Esta husomwa hadharani.
Mwandishi
Mwandishi hajulikani, lakini inadhaniwa alikuwa ni Mordekai. Wengine hudhani ni Ezra au Nehemia kwa sababu ya mtindo wa kuandika.
Kusudi
Kuonesha ukuu wa Mungu, na upendo wake kwa watu wake.
Mahali
Katika jumba la kifalme huko Shushani, mji mkuu wa Uajemi.
Tarehe
Kama mwaka wa 470 K.K.
Wahusika Wakuu
Esta, Mordekai, Mfalme Ahasuero, na Hamani.
Wazo Kuu
Mungu aliwaokoa Wayahudi katika maangamizi yaliyopangwa na Hamani. Mungu aligeuza mabaya yaliyokusudiwa dhidi ya Wayahudi yakawapata adui zao katika utawala wote wa Mfalme Ahasuero, baada ya Esta na watu wake kumwomba Mungu.
Mambo Muhimu
Esta kuchaguliwa kuwa malkia badala ya Vashti aliyekuwa malkia kabla yake, na jinsi Mungu alivyobadilisha makusudi ya Hamani dhidi ya Wayahudi.
Yaliyomo
Esta afanywa malkia (1:1–2:23)
Hamani, Mordekai na Esta (3:1–7:10)
Ushindi wa Wayahudi (8:1–10:3).

Iliyochaguliwa sasa

Esta Utangulizi: NENO

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia