Kutoka 17:6-7
Kutoka 17:6-7 NEN
Huko nitasimama mbele yako karibu na mwamba wa Horebu. Uupige mwamba na maji yatatoka ndani yake kwa ajili ya watu kunywa.” Kwa hiyo Mose akafanya haya mbele ya wazee wa Israeli. Naye akapaita mahali pale Masa, na Meriba kwa sababu Waisraeli waligombana na kumjaribu BWANA wakisema, “Je, BWANA yu pamoja nasi au la?”