Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Kutoka 34:29-35

Kutoka 34:29-35 NENO

Musa alipoteremka kutoka Mlima Sinai akiwa na vile vibao viwili vya Ushuhuda mikononi mwake, hakujua kuwa uso wake ulikuwa uking’aa, kwa sababu alikuwa amezungumza na Mwenyezi Mungu. Haruni na Waisraeli wote walipomwona Musa, kuwa uso wake unang’aa, waliogopa kumkaribia. Lakini Musa akawaita, kwa hiyo Haruni na viongozi wote wa jumuiya wakarudi, naye akazungumza nao. Baadaye Waisraeli wote wakamkaribia, naye akawapa amri zote Mwenyezi Mungu alizompa katika Mlima Sinai. Musa alipomaliza kuzungumza nao, akaweka utaji kwenye uso wake. Lakini kila wakati Musa alipoingia mbele za Mwenyezi Mungu kuzungumza naye, aliondoa ule utaji hadi alipotoka nje. Naye alipotoka nje na kuwaambia Waisraeli lile ambalo ameagizwa, waliona kuwa uso wake unang’aa. Kisha Musa angerudisha utaji juu ya uso wake hadi alipoingia ili kuzungumza na Mwenyezi Mungu.