Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Kutoka 40:34-38

Kutoka 40:34-38 NENO

Ndipo wingu likafunika Hema la Kukutania, na utukufu wa Mwenyezi Mungu ukaijaza maskani ya Mungu. Musa hakuweza kuingia ndani ya Hema la Kukutania kwa sababu wingu lilikuwa limetua juu ya Hema, nao utukufu wa Mwenyezi Mungu ukaijaza maskani ya Mungu. Katika safari yote ya Waisraeli, kila wakati wingu lilipoinuka kutoka juu ya maskani ya Mungu, wangeondoka; lakini kama wingu halikuinuka, hawakuondoka, hadi siku lilipoinuka. Kwa hiyo wingu la Mwenyezi Mungu lilikuwa juu ya maskani ya Mungu mchana, na moto ulikuwa katika hilo wingu wakati wa usiku, machoni pa nyumba yote ya Israeli siku zote za safari zao.