Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Ezekieli 14:1-11

Ezekieli 14:1-11 NENO

Baadhi ya wazee wa Israeli walinijia na kuketi mbele yangu. Ndipo neno la Mwenyezi Mungu likanijia kusema: “Mwanadamu, watu hawa wameweka sanamu katika mioyo yao na kuweka vitu viovu vya kukwaza mbele ya macho yao. Je, kweli niwaruhusu waniulize jambo lolote? Kwa hiyo sema nao uwaambie, ‘Hili ndilo asemalo Bwana Mungu Mwenyezi: Mwisraeli yeyote anapoweka sanamu moyoni mwake na kuweka kitu kiovu cha kukwaza mbele ya macho yake na kisha akaenda kwa nabii, Mimi Mwenyezi Mungu nitamjibu peke yangu sawasawa na ukubwa wa ibada yake ya sanamu. Nitafanya jambo hili ili kukamata tena mioyo ya watu wa Israeli, ambao wote wameniacha kwa ajili ya sanamu zao.’ “Kwa hiyo iambie nyumba ya Israeli, ‘Hili ndilo asemalo Bwana Mungu Mwenyezi: Tubuni! Acheni sanamu zenu, na matendo yenu yote ya machukizo! “ ‘Mwisraeli au mgeni yeyote anayeishi Israeli anapojitenga nami, na kujiwekea sanamu moyoni mwake, na hivyo kuweka kitu kiovu cha kukwaza mbele ya macho yake, na kisha akamwendea nabii kuuliza shauri kwangu, Mimi Mwenyezi Mungu nitamjibu mwenyewe. Nitamkabili mtu huyo na kumwadhibu, na kumfanya ishara na mithali. Nitamkatilia mbali kutoka kwa watu wangu. Ndipo mtajua kuwa Mimi ndimi Mwenyezi Mungu. “ ‘Na ikiwa nabii ameshawishika kutoa unabii, Mimi Mwenyezi Mungu nitakuwa nimemshawishi nabii huyo; nami nitaunyoosha mkono wangu dhidi yake na kumwangamiza kutoka miongoni mwa watu wangu Israeli. Watawajibika kwa hatia yao: nabii atakuwa na hatia sawa na yule mtu aliyekuja kuuliza neno kwake. “ ‘Ndipo watu wa Israeli hawataniacha tena, wala kujitia unajisi tena kwa dhambi zao zote. Watakuwa watu wangu, nami nitakuwa Mungu wao, asema Bwana Mungu Mwenyezi.’ ”