Wagalatia Utangulizi
Utangulizi
Paulo aliandika waraka huu katika safari yake ya kwanza kueneza Injili. Baada yake kuondoka Galatia, waumini Wayahudi walifika huko, nao wakaanza kusisitiza kwamba lazima watu wa Mataifa walioamini kwanza watimize Torati ya Musa ili wapate kuokoka. Paulo aliandika kupinga mafundisho hayo, akionesha jinsi Ibrahimu, ambaye aliishi miaka 400 kabla ya Torati ya Musa kutolewa, alivyookolewa kwa imani. Alionesha kwamba kama vile Torati haingeweza kumwokoa mtu, basi hakuna mtu angeweza kuwa mkamilifu kwa kujitahidi kwa uwezo wake mwenyewe kuitimiza Torati.
Mwandishi
Mtume Paulo.
Kusudi
Kukataa mafundisho ya kuwa muumini wa Mataifa ni lazima atii Torati ndio aokolewe.
Mahali
Antiokia.
Tarehe
Mnamo 49 B.K.
Wahusika Wakuu
Paulo, Tito, Barnaba, Petro, na walimu wa uongo.
Wazo Kuu
Paulo anatetea kwa bidii kweli ya Injili ambayo kiini chake ni kwamba, “Mtu anaokolewa kwa neema ya Mwenyezi Mungu kwa kumwamini Al-Masihi.”
Mambo Muhimu
Paulo anasisitiza uhalali wa Injili, ubora wa Injili, na uhuru wa Injili.
Yaliyomo
Paulo atetea Injili na mamlaka yake kama mtume (1:1–2:21)
Kuwekwa huru kutokana na Torati (3:1–4:31)
Uhuru wa mfuasi wa Al-Masihi (5:1-26)
Mawaidha kuhusu mwenendo wa mfuasi wa Al-Masihi (6:1-18).
Iliyochaguliwa sasa
Wagalatia Utangulizi: NENO
Kuonyesha
Shirikisha
Nakili
Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia
Neno: Maandiko Matakatifu™ NMM™
Hakimiliki © 2018, 2024 na Biblica, Inc.
Imetumiwa kwa ruhusa.
Haki zote zimehifadhiwa duniani kote.
Kiswahili Contemporary Scriptures™
Copyright © 2018, 2024 by Biblica, Inc.
Used with permission. All rights reserved worldwide.