Mwanzo 1:1-5
Mwanzo 1:1-5 NENO
Hapo mwanzo Mungu aliumba mbingu na dunia. Wakati huu dunia ilikuwa haina umbo, tena ilikuwa tupu. Giza lilikuwa juu ya vilindi vya maji, naye Roho wa Mungu alikuwa ametulia juu ya maji. Mungu akasema, “Iwepo nuru,” nayo nuru ikawepo. Mungu akaona ya kuwa nuru ni njema; ndipo Mungu akatenganisha nuru na giza. Mungu akaiita nuru “mchana”, na giza akaliita “usiku”. Ikawa jioni, ikawa asubuhi, siku ya kwanza.