Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Mwanzo 13:14-18

Mwanzo 13:14-18 NENO

Baada ya Lutu kuondoka, Mwenyezi Mungu akamwambia Abramu, “Ukiwa hapo ulipo, inua macho yako utazame kaskazini na kusini, mashariki na magharibi. Nchi yote unayoiona nitakupa wewe na uzao wako hata milele. Nitaufanya uzao wako uwe mwingi kama mavumbi ya nchi, hivyo ikiwa kuna yeyote awezaye kuhesabu mavumbi, basi uzao wako utahesabika. Ondoka, tembea katika marefu na mapana ya nchi, kwa maana ninakupa wewe.” Basi Abramu akaondoa mahema yake, akaenda kuishi karibu na mialoni ya Mamre huko Hebroni. Naye akamjengea Mwenyezi Mungu madhabahu huko.