Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Hagai 2:20-23

Hagai 2:20-23 NENO

Neno la Mwenyezi Mungu likamjia Hagai kwa mara ya pili katika siku ya ishirini na nne ya mwezi kusema: “Mwambie Zerubabeli mtawala wa Yuda kwamba nitazitikisa mbingu na nchi. Nitapindua viti vya falme, na kuziharibu kabisa nguvu za falme za kigeni. Nitapindua magari ya vita pamoja na waendeshaji wake; farasi na wapanda farasi wataanguka, kila mmoja kwa upanga wa ndugu yake. “ ‘Katika siku ile,’ asema Mwenyezi Mungu, Mungu wa majeshi ya mbinguni, ‘nitakuchukua wewe, mtumishi wangu Zerubabeli mwana wa Shealtieli,’ asema Mwenyezi Mungu. ‘Nitakufanya kama pete yangu ya muhuri, kwa kuwa nimekuchagua,’ asema Mwenyezi Mungu, Mungu wa majeshi ya mbinguni.”

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha