Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Waebrania 10:11-18

Waebrania 10:11-18 NENO

Kila kuhani husimama siku kwa siku akifanya huduma yake ya ibada, na kutoa tena na tena dhabihu zile zile, ambazo haziwezi kamwe kuondoa dhambi. Lakini huyu kuhani baada ya kutoa dhabihu moja kwa ajili ya dhambi kwa wakati wote, aliketi mkono wa kuume wa Mungu. Tangu wakati huo anangoja hadi adui zake wawekwe chini ya miguu yake, kwa sababu kwa dhabihu moja amewafanya wakamilifu milele wale wote wanaotakaswa. Pia Roho wa Mungu anatushuhudia kuhusu jambo hili. Kwanza anasema: “Hili ndilo agano nitakalofanya nao baada ya siku hizo, asema Mwenyezi Mungu. Nitaziweka sheria zangu mioyoni mwao, na kuziandika katika nia zao.” Kisha aongeza kusema: “Dhambi zao na kutokutii kwao sitakumbuka tena.” Basi haya yaliposamehewa, hakuna tena dhabihu yoyote inayohitajika kwa ajili ya dhambi.