Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Waebrania 6:9-15

Waebrania 6:9-15 NEN

Ingawa tunasema hivi, ndugu zangu wapendwa, kwa upande wenu tuna hakika ya mambo mema zaidi, mambo yale yahusuyo wokovu. Mungu si mdhalimu: yeye hataisahau kazi yenu na upendo ule mlioonyesha kwa ajili yake katika kuwahudumia watakatifu na hata sasa mnaendelea kuwahudumia. Nasi twataka kila mmoja wenu aonyeshe bidii iyo hiyo ili mpate kujua uhakika kamili wa lile tumaini mpaka mwisho, ili msije mkawa wavivu, bali mpate kuwaiga wale ambao kwa imani na saburi hurithi zile ahadi. Mungu alipompa Abrahamu ahadi yake, kwa kuwa hakuwepo mwingine aliyekuwa mkuu kuliko yeye ambaye angeweza kuapa kwa jina lake, aliapa kwa nafsi yake, akisema, “Hakika nitakubariki na kukupa wazao wengi.” Abrahamu naye, baada ya kungoja kwa saburi, alipokea kile kilichoahidiwa.

Mipango ya Kusoma Bila Malipo na Ibada zinazohusiana na Waebrania 6:9-15