Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Hosea 3

3
Upatanisho wa Hosea na mkewe
1Mwenyezi Mungu akaniambia, “Nenda, ukaoneshe upendo wako kwa mke wako tena, ingawa amependwa na mwingine naye ni mzinzi. Mpende kama Mwenyezi Mungu apendavyo Waisraeli, ingawa wanageukia miungu mingine na kupenda mikate mitamu ya zabibu kavu iliyowekwa wakfu.”
2Basi nilimnunua huyo mwanamke kwa shekeli kumi na tano#3:2 Shekeli 15 ni sawa na gramu 170. za fedha, pia kwa kiasi kama cha homeri moja na nusu#3:2 Homeri moja na nusu ni kama lita 330. ya shayiri. 3Kisha nilimwambia, “Utaishi nami kwa siku nyingi, hupaswi kuwa kahaba au kuwa na uhusiano wa karibu na mtu yeyote, nami nitaishi na wewe.”
4Kwa maana Waisraeli wataishi siku nyingi bila kuwa na mfalme wala mkuu, bila kuwa na dhabihu wala mawe matakatifu, bila kizibau wala miungu ya nyumbani. 5Baadaye Waisraeli watarudi na kumtafuta Mwenyezi Mungu, Mungu wao, na Daudi mfalme wao. Watakuja wakitetemeka kwa Mwenyezi Mungu na kwa baraka zake katika siku za mwisho.

Iliyochaguliwa sasa

Hosea 3: NENO

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia