Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Hosea Utangulizi

Utangulizi
Hosea mwana wa Beeri alikuwa mzaliwa wa Ufalme wa Kaskazini, yaani Israeli, ambao pia uliitwa Efraimu. Maana ya jina Hosea ni “Wokovu”. Huduma ya Hosea kwa Ufalme wa Kaskazini ilikaribiana sana na ile ya Amosi. Hawa wawili ndio manabii pekee wa vitabu vya Manabii ambao vitabu vyao vilihusu Ufalme wa Kaskazini na maangamizi yake.
Hosea alianza huduma yake miaka ya baadaye ya utawala wa Yeroboamu wa Pili, wakati Israeli ikifurahia utulivu wa kisiasa na ustawi wa kiuchumi. Kufuatia kifo cha Yeroboamu wa Pili mnamo 753 K.K., hali ya taifa la Israeli ilibadilika. Amani na utulivu katika taifa vilitoweka. Taifa likaporomoka na kuangamia. Waisraeli wakapigwa na Waashuru na kisha kupelekwa uhamishoni mnamo 722 K.K.
Mwandishi
Hosea.
Kusudi
Kuonesha upendo mkuu wa Mwenyezi Mungu kwa Waisraeli waliokuwa wamemwasi. Watu wanapomwacha na kumwasi, Mwenyezi Mungu anaendelea kuwapenda na kuwarejesha kwake.
Mahali
Ufalme wa Kaskazini yaani Israeli, ambao uliitwa Efraimu.
Tarehe
Mnamo 715–710 K.K.
Wahusika Wakuu
Hosea, Gomeri, na watoto wao.
Wazo Kuu
Hukumu na upendo mkuu wa Mwenyezi Mungu kwa watu wake.
Mambo Muhimu
Hosea anaelezea hali ya taifa la Israeli akitumia hali iliyojitokeza katika maisha ya kila siku. Mwenyezi Mungu anafananishwa na: mume, baba, simba, chui, dubu, umande, mvua, nondo, na mifano mingine. Israeli inafananishwa na: mke aliyekosa uaminifu kwa mumewe, mtu mgonjwa, mzabibu, mzeituni, mwanamke anayejifungua, jiko la kuokea, ukungu wa asubuhi, makapi, moshi, na mifano mingine.
Yaliyomo
Maisha ya Hosea katika jamii (1:1–3:5)
Hali ya dhambi ya Israeli (4:1–10:15)
Hukumu ya Mwenyezi Mungu na rehema zake (11:1–14:9).

Iliyochaguliwa sasa

Hosea Utangulizi: NENO

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia