Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Isaya 14:1-8

Isaya 14:1-8 NENO

BWANA atamhurumia Yakobo, atamchagua Israeli tena, na kuwakalisha katika nchi yao wenyewe. Wageni wataungana nao na kujiunga na nyumba ya Yakobo. Mataifa watawachukua na kuwaleta mahali pao wenyewe. Nayo nyumba ya Israeli itamiliki mataifa kama watumishi na wajakazi katika nchi ya BWANA. Watawafanya watekaji wao kuwa mateka, na kuwatawala waliowadhulumu. Katika siku BWANA atakapokuondolea mateso, udhia na utumwa wa kikatili, utaichukua dhihaka hii dhidi ya mfalme wa Babeli: Tazama jinsi mtesi alivyofikia mwisho! Tazama jinsi ghadhabu yake kali ilivyokoma! BWANA amevunja fimbo ya mwovu, fimbo ya utawala ya watawala, ambayo kwa hasira waliyapiga mataifa kwa mapigo yasiyo na kikomo, nao kwa ghadhabu kali waliwatiisha mataifa kwa jeuri pasipo huruma. Nchi zote ziko kwenye mapumziko na kwenye amani, wanabubujika kwa kuimba. Hata misunobari na mierezi ya Lebanoni inashangilia mbele yako na kusema, “Basi kwa kuwa umeangushwa chini, hakuna mkata miti atakayekuja kutukata.”