Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Yakobo Utangulizi

Utangulizi
Waraka wa Yakobo unaweza kuwa mojawapo ya nyaraka za kwanza kabisa katika Agano Jipya. Inawezekana uliandikwa wakati moja na ule wa Paulo kwa Wagalatia. Waraka huu uliandikiwa Wakristo wa Kiyahudi wa utawanyiko, waliokuwa katika hali ya ugeni huko Ponto, Galatia, Kapadokia, Asia na Bithinia ili kuwapa mawaidha kuhusu ilivyowapasa kuishi kama waumini, wakidhihirishwa na matendo mema na imani itendayo kazi. Barua hii ina mithali nyingi fupi fupi zinazosaidia kuweka wazi yale Mafundisho ya Mlimani ya Bwana Yesu.
Matatizo yanayozungumziwa yalikuwa yakiwasumbua waumini. Tunasoma juu ya kiburi, ubaguzi, choyo, tamaa, unafiki, kupenda anasa, na kusengenya. Yakobo aliandika kusahihisha makosa haya kwa kuonyesha kwamba imani pasipo matendo imekufa. Hii ina maana kuwa kusema tu kwamba unaamini hakutoshi, bali imani halisi huambatana na matendo.
Mwandishi
Yakobo, ndugu yake Yesu.
Kusudi
Kuwahimiza waumini kufanya mabadiliko yanayohitajika katika maisha ya Mkristo.
Mahali
Yerusalemu.
Tarehe
Kama mwaka wa 49 B.K.
Wahusika Wakuu
Yakobo, na Wayahudi wa Utawanyiko.
Wazo Kuu
Yakobo anasisitiza umuhimu wa Mkristo kuishi maisha yanayodhihirisha hali yake ya ndani. Hapo ndipo ulimwengu utapata kujua jinsi Injili iwezavyo kubadili maisha ya watu.
Mambo Muhimu
Imani pasipo matendo imekufa; ili kuitimiza sheria ya upendo lazima imani yetu iwe na matendo. Yakobo anawafundisha Wakristo kutokubaliana na hali ya kidunia kuhusu mali na utajiri. Wakristo wanatakiwa kujiwekea hazina kwa Mungu, hivyo Wakristo hawapaswi kuwapendelea wenye mali, wala kuwadharau maskini. Pia waombe hekima kutoka kwa Mungu.
Mgawanyo
Maisha ya imani ya kweli (1:1-27)
Matarajio ya watu wasioamini kwa Wakristo (2:1-13)
Imani ya kweli na matendo (2:14-26)
Kuutawala ulimi (3:1-18)
Mwenendo upasao (4:1-17)
Matajiri wakemewa (5:1-6)
Mawaidha ya mwisho (5:7-20).

Iliyochaguliwa sasa

Yakobo Utangulizi: NEN

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia