Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Yeremia 29:7-14

Yeremia 29:7-14 NEN

Pia tafuteni amani na mafanikio ya mji ambamo nimewapeleka uhamishoni. Mwombeni BWANA kwa ajili ya mji huo, kwa sababu ukistawi, ninyi pia mtastawi.” Naam, hili ndilo BWANA Mwenye Nguvu Zote, Mungu wa Israeli, asemalo: “Msikubali manabii na wabashiri walioko miongoni mwenu wawadanganye. Msisikilize ndoto ambazo mmewatia moyo kuota. Wanawatabiria ninyi uongo kwa jina langu. Sikuwatuma,” asema BWANA. Hili ndilo asemalo BWANA: “Miaka sabini itakapotimia kwa ajili ya Babeli, nitakuja kwenu na kutimiza ahadi yangu ya rehema ya kuwarudisha mahali hapa. Kwa maana ninajua mipango niliyo nayo kwa ajili yenu,” asema BWANA, “ni mipango ya kuwafanikisha na wala si ya kuwadhuru, ni mipango ya kuwapa tumaini katika siku zijazo. Kisha mtaniita, na mtakuja na kuniomba, nami nitawasikiliza. Mtanitafuta na kuniona, mtakaponitafuta kwa moyo wenu wote. Nitaonekana kwenu,” asema BWANA, “nami nitawarudisha watu wenu waliotekwa. Nitawakusanya kutoka mataifa yote na mahali pote nilipokuwa nimewafukuzia, nami nitawarudisha mahali ambapo nilikuwa nimewatoa walipochukuliwa uhamishoni,” asema BWANA.

Mipango ya Kusoma Bila Malipo na Ibada zinazohusiana na Yeremia 29:7-14