Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Ayubu 26

26
Hotuba ya tisa ya Ayubu
Ayubu anajibu: Utukufu wa Mwenyezi Mungu hauchunguziki
1Kisha Ayubu akajibu:
2“Tazama jinsi ulivyomsaidia mtu asiye na uwezo!
Jinsi ulivyouokoa mkono ulio dhaifu!
3Ni shauri gani ulilompa yeye asiye na hekima?
Nayo ni busara gani kubwa uliyoonesha!
4Ni nani aliyekusaidia kutamka maneno hayo?
Nayo ni roho ya nani iliyosema kutoka kinywani mwako?
5“Wafu wako katika maumivu makuu,
wale walio chini ya maji,
na wale wanaoishi ndani yake.
6Mauti#26:6 yaani Kuzimu; Kiebrania ni Sheol iko wazi mbele za Mungu;
Uharibifu#26:6 kwa Kiebrania ni Abadon haukufunikwa.
7Hutandaza anga la kaskazini mahali patupu;
naye huining’iniza dunia mahali pasipo na kitu.
8Huyafungia maji kwenye mawingu yake,
hata hivyo mawingu hayapasuki kwa uzito wake.
9Huufunika uso wa mwezi mpevu,
akitandaza mawingu juu yake.
10Amechora mstari wa upeo juu ya maji,
ameweka mpaka wa nuru na giza.
11Nguzo za mbingu nazo zatetemeka,
zinatishika anapozikemea.
12Kwa nguvu zake aliisukasuka bahari;
kwa hekima yake alimkata Rahabu#26:12 Rahabu hapa ni fumbo la kumaanisha Lewiathani, mnyama mkubwa wa baharini mwenye magamba anayefanana na joka kubwa, mwenye umbo la kutisha, asiyeweza kuvuliwa. vipande vipande.
13Aliisafisha anga kwa pumzi yake;
kwa mkono wake alimchoma joka aendaye mbio.
14Haya ni mambo madogo tu katika matendo yake;
tazama jinsi ulivyo mdogo mnong’ono tunaousikia kumhusu!
Ni nani basi awezaye kuelewa
ngurumo za nguvu zake?”

Iliyochaguliwa sasa

Ayubu 26: NENO

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia