Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Ayubu 32:6-9

Ayubu 32:6-9 NENO

Basi Elihu mwana wa Barakeli wa kabila la Buzi akasema: “Mimi ni mdogo kwa umri, nanyi ni wazee; ndiyo sababu niliogopa, sikuthubutu kuwaambia kile ninachojua. Nilifikiri, ‘Yafaa umri useme, nao wingi wa miaka ungefundisha hekima.’ Lakini ni Roho iliyo ndani ya mwanadamu, pumzi ya Mwenyezi, ndiyo impayo ufahamu. Sio wazee peke yao walio na hekima, sio wenye umri mkubwa peke yao wanaofahamu lililo sawa.