Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Yoeli 3:1-13

Yoeli 3:1-13 NENO

“Katika siku hizo na wakati huo, nitakaporejesha neema ya Yuda na Yerusalemu, nitayakusanya mataifa yote na kuyaleta katika Bonde la Yehoshafati. Hapo nitaingia kwenye hukumu dhidi yao kuhusu urithi wangu, watu wangu Israeli, kwa kuwa waliwatawanya watu wangu miongoni mwa mataifa na kuigawa nchi yangu. Waliwapigia kura watu wangu na kuwauza wavulana ili kupata makahaba; waliwauza wasichana ili wapate kunywa mvinyo. “Sasa una nini dhidi yangu, ee Tiro na Sidoni, nanyi nchi zote za Ufilisti? Je, mnanilipiza kwa yale niliyoyafanya? Kama mnalipa, mimi nitalipiza juu ya vichwa vyenu kwa kasi na kwa haraka yale mliyoyatenda. Kwa kuwa mlichukua fedha na dhahabu yangu pia mkabeba hazina zangu nzuri sana mkapeleka kwenye mahekalu yenu. Mliwauza watu wa Yuda na Yerusalemu kwa Wayunani, ili mpate kuwapeleka mbali na nchi yao. “Tazama nitawaamsha kutoka zile sehemu mlizowauza, nami nitawalipiza juu ya vichwa vyenu kile mlichofanya. Nitawauza wana wenu wa kiume na wa kike kwa watu wa Yuda, nao watawauza kwa Waseba, taifa lililo mbali.” Mwenyezi Mungu amesema. Tangazeni hili miongoni mwa mataifa: Jiandaeni kwa vita! Amsha mashujaa! Wapiganaji wote wasogee karibu na kushambulia. Majembe yenu yafueni yawe panga, na miundu yenu ya kukatia iwe mikuki. Aliye dhaifu na aseme, “Mimi nina nguvu!” Njooni haraka, ninyi mataifa yote kutoka pande zote, kusanyikeni huko. Shusha mashujaa wako, Ee Mwenyezi Mungu! “Mataifa na yaamshwe; na yasonge mbele kuelekea Bonde la Yehoshafati, kwa kuwa nitaketi mahali pale kuhukumu mataifa yote yaliyo kila upande. Tia mundu, kwa kuwa mavuno yamekomaa. Njooni, mkanyage zabibu, kwa kuwa shinikizo la kukamulia zabibu limejaa na mapipa yanafurika: kwa kuwa uovu wao ni mkubwa!”