Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Yona Utangulizi

Utangulizi
Jina Yona maana yake ni “Hua”. Kitabu hiki kinaelezea yale yaliyomtokea Yona kama mjumbe wa Mwenyezi Mungu. Yona alikuwa ameagizwa na Mwenyezi Mungu aende kuwaonya watu wa Ninawi juu ya hukumu iliyokuwa inakuja. Alijaribu kumkimbia Mwenyezi Mungu na kuelekea Tarshishi, upande wa magharibi wa Israeli badala ya kuelekea Ninawi iliyokuwa kaskazini mashariki. Yona alitupwa baharini akamezwa na samaki mkubwa sana ambaye alimtapika pwani ya mashariki mwa Bahari ya Kati (Mediterania). Hatimaye alikwenda Ninawi na kuwaonya watu kuhusu hukumu ya Mwenyezi Mungu na watu wa Ninawi walitubu. Badala ya kufurahia jambo hili, Yona alihuzunika na kuvunjika moyo kwa sababu Mwenyezi Mungu alionesha rehema na kughairi hukumu dhidi ya watu wa Ninawi.
Mwandishi
Yona mwana wa Amitai.
Kusudi
Kuonesha ukuu wa rehema za Mwenyezi Mungu na wokovu kwa mwanadamu. Pia, kuonesha jinsi ambavyo mwanadamu hawezi kukimbia wito wa Mwenyezi Mungu.
Mahali
Inaweza kuwa Israeli au Ninawi.
Tarehe
Inadhaniwa kuwa mnamo 785–760 K.K.
Wahusika Wakuu
Yona, nahodha wa meli na mabaharia, mfalme wa Ninawi, na Waninawi wote.
Wazo Kuu
Ukuu wa rehema za Mwenyezi Mungu.
Mambo Muhimu
Rehema za Mwenyezi Mungu na upendo wa Mwenyezi Mungu kwa watu wote.
Yaliyomo
Yona amkimbia Mwenyezi Mungu (1:1-17)
Maombi ya Yona na kuokolewa (2:1-10).
Yona aenda Ninawi (3:1-10)
Hasira ya Yona kwa ajili ya huruma ya Mwenyezi Mungu (4:1-11).

Iliyochaguliwa sasa

Yona Utangulizi: NENO

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia