Yoshua 19
19
Mgawo kwa Simeoni
1Kura ya pili ikaangukia kabila la Simeoni, kufuatana na koo zao. Urithi wao ulikuwa ndani ya eneo la Yuda. 2Ulijumuisha:
Beer-Sheba (au Sheba), Molada, 3Hasar-Shuali, Bala, Esemu, 4Eltoladi, Bethuli, Horma, 5Siklagi, Beth-Markabothi, Hasar-Susa, 6Beth-Lebaothi na Sharuheni; hii ilikuwa miji kumi na tatu pamoja na vijiji vyake.
7Pia Aini, Rimoni, Etheri, na Ashani; hii ilikuwa miji minne na vijiji vyake, 8pamoja na vijiji vyote vinavyoizunguka miji hii hadi Baalath-Beeri (ambayo ndiyo Rama iliyo katika Negebu).
Huu ulikuwa ni urithi wa kabila la Simeoni kufuatana na koo zao. 9Urithi wa Wasimeoni ulitolewa kutoka fungu la Yuda, kwa kuwa fungu la Yuda lilikuwa kubwa kuliko walivyohitaji. Hivyo kabila la Simeoni lilipewa urithi wao ndani ya eneo la Yuda.
Mgawo kwa Zabuloni
10Kura ya tatu ikaangukia kabila la Zabuloni, kufuatana na koo zao:
Mpaka wa urithi wao uliendelea hadi Saridi. 11Kuelekea upande wa magharibi ukafika Marala, ukagusa Dabeshethi, na kuendelea hadi kwenye bonde karibu na Yokneamu. 12Ukageuka mashariki, kuanzia Saridi kuelekea mawio ya jua hadi kwenye nchi ya Kisiloth-Tabori, na kwenda hadi Daberathi, kupanda Yafia. 13Kisha ukaendelea mashariki hadi Gath-Heferi na kufika Eth-Kasini, ukatokea Rimoni na kugeuka kuelekea Nea. 14Huko mpaka ukazungukia upande wa kaskazini hadi Hanathoni na kuishia katika Bonde la Ifta-Eli.
15Miji mingine iliyojumuishwa ni Katathi, Nahalali, Shimroni, Idala na Bethlehemu. Kulikuwa na miji kumi na mbili pamoja na vijiji vyake.
16Miji hii na vijiji vyake ilikuwa urithi wa Zabuloni, kufuatana na koo zao.
Mgawo kwa Isakari
17Kura ya nne ikaangukia kabila la Isakari, kufuatana na koo zao. 18Eneo lao lilijumuisha:
Yezreeli, Kesulothi, Shunemu, 19Hafaraimu, Shioni, Anaharathi, 20Rabithi, Kishioni, Ebesi, 21Remethi, En-Ganimu, En-Hada na Beth-Pasesi.
22Mpaka ule ukagusa Tabori, Shahasuma na Beth-Shemeshi, na ukaishia kwenye Yordani.
Ilikuwa miji kumi na sita, pamoja na vijiji vyake.
23Miji hii pamoja na vijiji vyake ilikuwa urithi wa kabila la Isakari, kufuatana na koo zao.
Mgawo kwa Asheri
24Kura ya tano ikaangukia kabila la Asheri, kufuatana na koo zao. 25Eneo lao lilijumuisha:
Helkathi, Hali, Beteni, Akshafu, 26Alameleki, Amadi na Mishali. Upande wa magharibi mpaka uligusa Karmeli na Shihor-Libnathi. 27Tena ukageuka mashariki kuelekea Beth-Dagoni, ukagusa Zabuloni na Bonde la Ifta-Eli, ukaenda upande wa kaskazini hadi Beth-Emeki na Neyeli, ukipitia Kabul upande wa kushoto. 28Ukaendelea hadi Abdoni, Rehobu, Hamoni na Kana, na kufika Sidoni Kuu. 29Mpaka huo ukageukia nyuma kuelekea Rama na kwenda hadi kwenye mji wenye ngome wa Tiro, ukageuka kuelekea Hosa na kutokeza baharini katika eneo la Akzibu, 30Uma, Afeki na Rehobu.
Ilikuwa miji ishirini na mbili, pamoja na vijiji vyake.
31Miji hii pamoja na vijiji vyake ilikuwa urithi wa kabila la Asheri, kufuatana na koo zao.
Mgawo kwa Naftali
32Kura ya sita ikaangukia kabila la Naftali, kufuatana na koo zao:
33Mpaka wao uliendelea kutoka Helefi na kwenye mwaloni ulio Saananimu, ukipitia Adami-Nekebu na Yabineeli hadi Lakumu, na kuishia katika Mto Yordani. 34Mpaka ukaendelea magharibi kupitia Aznoth-Tabori na kutokea Hukoki. Ukagusa Zabuloni upande wa kusini, Asheri upande wa magharibi, na Yordani upande wa mashariki.
35Miji yenye ngome ilikuwa Sidimu, Seri, Hamathi, Rakathi, Kinerethi, 36Adama, Rama, Hazori, 37Kedeshi, Edrei, na En-Hasori, 38Ironi, Migdal-Eli, Horemu, Beth-Anathi na Beth-Shemeshi.
Kulikuwa na miji kumi na tisa na vijiji vyake.
39Miji hiyo pamoja na vijiji vyake ilikuwa urithi wa kabila la Naftali, kufuatana na koo zao.
Mgawo kwa Dani
40Kura ya saba ikaangukia kabila la Dani, kufuatana na koo zao. 41Eneo la urithi wao lilijumuisha:
Sora, Eshtaoli, Iri-Shemeshi, 42Shaalabini, Aiyaloni, Ithla, 43Eloni, Timna, Ekroni, 44Elteke, Gibethoni, Baalathi, 45Yehudi, Bene-Beraki, Gath-Rimoni, 46Me-Yarkoni na Rakoni, pamoja na eneo linalotazamana na Yafa.
47(Lakini Wadani walipata shida kulimiliki eneo lao; kwa hiyo walipanda kuishambulia Leshemu, wakaitwaa, wakawaua watu wake kwa upanga na kuukalia. Walikaa Leshemu na kuuita Dani kufuatana na jina la baba yao.)
48Miji hii na vijiji vyake ilikuwa urithi wa kabila la Dani, kufuatana na koo zao.
Mgawo kwa Yoshua
49Walipomaliza kuigawa nchi kulingana na sehemu zilizowaangukia, Waisraeli walimpa Yoshua mwana wa Nuni urithi kati yao, 50kama vile Mwenyezi Mungu alivyokuwa ameamuru. Walimpa mji alioutaka, ambao ni Timnath-Sera#19:50 Unajulikana pia kama Timnath-Heresi(taz. Yoshua 24:30; Waamuzi 2:9). ulio katika nchi ya vilima ya Efraimu. Naye akajenga mji, akakaa huko.
51Haya ndio maeneo ambayo kuhani Eleazari, Yoshua mwana wa Nuni, na viongozi wa koo za makabila ya Israeli waliyagawanya kwa kura huko Shilo mbele za Mwenyezi Mungu, penye ingilio la Hema la Kukutania. Hivyo wakamaliza kuigawanya nchi.
Iliyochaguliwa sasa
Yoshua 19: NENO
Kuonyesha
Shirikisha
Nakili

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia
Neno: Maandiko Matakatifu™ NMM™
Hakimiliki © 2018, 2024 na Biblica, Inc.
Imetumiwa kwa ruhusa.
Haki zote zimehifadhiwa duniani kote.
Kiswahili Contemporary Scriptures™
Copyright © 2018, 2024 by Biblica, Inc.
Used with permission. All rights reserved worldwide.