Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Yoshua 22:1-5

Yoshua 22:1-5 NENO

Ndipo Yoshua akawaita Wareubeni, Wagadi na nusu ya kabila la Manase, naye akawaambia, “Mmeshafanya yale yote Musa mtumishi wa Mwenyezi Mungu aliyowaamuru, nanyi mmenitii kwa kila jambo nililowaamuru. Kwa muda mrefu sasa, hadi siku hii ya leo, hamkuwaacha ndugu zenu, bali ninyi mmetimiza ile kazi Mwenyezi Mungu, Mungu wenu, aliyowapa. Sasa kwa kuwa Mwenyezi Mungu, Mungu wenu, amewapa ndugu zenu pumziko kama alivyoahidi, rudini nyumbani mwenu katika nchi ambayo Musa mtumishi wa Mwenyezi Mungu aliwapa ng’ambo ya Yordani. Lakini mwe waangalifu sana kushika amri na sheria ambazo Musa mtumishi wa Mwenyezi Mungu aliwapa: yaani kumpenda Mwenyezi Mungu, Mungu wenu, na kuenenda katika njia zake zote, kutii amri zake, kushikamana naye kwa uthabiti na kumtumikia kwa moyo wote na roho yote.”