Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Luka 17:11-19

Luka 17:11-19 NENO

Isa alipokuwa njiani akienda Yerusalemu, alipitia mpakani mwa Samaria na Galilaya. Alipokuwa akiingia kwenye kijiji kimoja, watu kumi waliokuwa na ukoma wakakutana naye. Wakasimama mbali, wakapaza sauti, wakasema, “Isa, Bwana, tuhurumie!” Alipowaona akawaambia, “Nendeni mkajioneshe kwa makuhani.” Nao walipokuwa njiani wakienda, wakatakasika. Mmoja wao alipoona kwamba amepona, akarudi kwa Isa, akimsifu Mungu kwa sauti kuu. Akajitupa miguuni mwa Isa akamshukuru. Yeye alikuwa Msamaria. Isa akauliza, “Je, hawakutakaswa wote kumi? Wako wapi wale wengine tisa? Hakuna hata mmoja aliyeonekana kurudi ili kumshukuru Mungu isipokuwa huyu mgeni?” Isa akamwambia, “Inuka na uende zako, imani yako imekuponya.”