Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Luka 21:29-38

Luka 21:29-38 NENO

Akawaambia mfano huu: “Uangalieni mtini na miti mingine yote. Inapochipua majani, ninyi wenyewe mnaweza kuona na kutambua wenyewe ya kuwa wakati wa kiangazi umekaribia. Vivyo hivyo, mnapoyaona mambo haya yakitukia, mtambue kwamba ufalme wa Mungu umekaribia. “Amin, nawaambia, kizazi hiki hakitapita hadi mambo haya yote yawe yametimia. Mbingu na nchi zitapita, lakini maneno yangu hayatapita kamwe. “Jihadharini mioyo yenu isije ikalemewa na anasa, ulevi na fadhaa za maisha haya, nayo siku ile ikawakuta ninyi bila kutazamia kama mtego unasavyo. Hivyo ndivyo siku hiyo itakavyowapata wanadamu wote wanaoishi katika uso wa dunia yote. Kesheni daima na mwombe ili mweze kuokoka na yale yote yatakayotokea na kusimama mbele ya Mwana wa Adamu.” Kila siku Isa alikuwa akifundisha Hekaluni, na jioni ilipofika, alienda zake kwenye Mlima wa Mizeituni na kukaa huko usiku kucha. Nao watu wote walikuja asubuhi na mapema Hekaluni ili kumsikiliza.