Mathayo 1
1
Kumbukumbu Za Ukoo Wa Yesu Kristo
(Luka 3:23-38)
1 Habari za ukoo wa Yesu Kristo mwana wa Daudi, mwana wa Abrahamu:
2 Abrahamu akamzaa Isaki,
Isaki akamzaa Yakobo,
Yakobo akawazaa Yuda na ndugu zake,
3 Yuda akawazaa Peresi na Zera, ambao mama yao alikuwa Tamari,
Peresi akamzaa Hesroni,
Hesroni akamzaa Aramu,
4Aramu akamzaa Aminadabu,
Aminadabu akamzaa Nashoni,
Nashoni akamzaa Salmoni,
5 Salmoni akamzaa Boazi, na mama yake Boazi alikuwa Rahabu,
Boazi akamzaa Obedi, ambaye mama yake alikuwa Ruthu,
Obedi akamzaa Yese,
6 Yese akamzaa Daudi ambaye alikuwa mfalme.
Daudi akamzaa Solomoni, ambaye mama yake ni yule aliyekuwa mke wa Uria.
7 Solomoni akamzaa Rehoboamu,
Rehoboamu akamzaa Abiya,
Abiya akamzaa Asa,
8Asa akamzaa Yehoshafati,
Yehoshafati akamzaa Yoramu,#1:8 Yoramu ndiye Yehoramu, maana yake ni Yehova yu juu.
Yoramu akamzaa Uzia,
9Uzia akamzaa Yothamu,
Yothamu akamzaa Ahazi,
Ahazi akamzaa Hezekia,
10 Hezekia akamzaa Manase,
Manase akamzaa Amoni,
Amoni akamzaa Yosia,
11 wakati wa uhamisho wa Babeli, Yosia alimzaa Yekonia na ndugu zake.
12 Baada ya uhamisho wa Babeli:
Yekonia alimzaa Shealtieli,
Shealtieli akamzaa Zerubabeli,
13Zerubabeli akamzaa Abiudi,
Abiudi akamzaa Eliakimu,
Eliakimu akamzaa Azori,
14Azori akamzaa Sadoki,
Sadoki akamzaa Akimu,
Akimu akamzaa Eliudi,
15Eliudi akamzaa Eleazari,
Eleazari akamzaa Matani,
Matani akamzaa Yakobo,
16 naye Yakobo akamzaa Yosefu ambaye alikuwa mumewe Maria, mama yake Yesu, aitwaye Kristo.#1:16 Kristo maana yake ni Masiya, yaani Aliyetiwa mafuta.
17Hivyo, kulikuwepo na jumla ya vizazi kumi na vinne tangu Abrahamu mpaka Daudi, vizazi kumi na vinne tangu Daudi hadi wakati wa uhamisho kwenda utumwani Babeli, na vizazi kumi na vinne tangu wakati wa uhamisho kwenda utumwani Babeli hadi Kristo.
Kuzaliwa Kwa Yesu Kristo
(Luka 2:1-7)
18 Basi Kuzaliwa kwake Yesu Kristo kulikuwa hivi: Maria mama yake alikuwa ameposwa na Yosefu, lakini kabla hawajakutana kimwili, Maria alionekana kuwa na mimba kwa uweza wa Roho Mtakatifu. 19 Kwa kuwa Yosefu, mwanaume aliyekuwa amemposa alikuwa mtu mwadilifu, hakutaka kumwaibisha Maria hadharani, aliazimu kumwacha kwa siri.
20 Lakini mara alipoazimu kufanya jambo hili, malaika wa Bwana akamtokea katika ndoto na kusema, “Yosefu mwana wa Daudi, usiogope kumchukua Maria awe mke wako, kwa maana mimba aliyo nayo ni kwa uweza wa Roho Mtakatifu. 21 Naye atamzaa mwana, nawe utamwita Jina lake Yesu,#1:21 Yesu ni Iesous kwa Kiyunani, na kwa Kiebrania ni Yoshua au Yeshua. Maana yake ni Yehova ni wokovu. kwa maana yeye ndiye atakayewaokoa watu wake kutoka dhambi zao.”
22 Haya yote yalitukia ili litimie lile Bwana alilokuwa amenena kupitia nabii, akisema: 23 “Tazama, bikira atachukua mimba, naye atamzaa mwana, nao watamwita Jina lake Imanueli”: maana yake, “Mungu pamoja nasi.”
24 Yosefu alipoamka kutoka usingizini, akafanya kama vile alivyoagizwa na malaika wa Bwana, akamchukua Maria kuwa mke wake. 25 Lakini hawakukutana kimwili mpaka Maria alipojifungua mwanawe kifungua mimba akamwita Jina lake Yesu.
Iliyochaguliwa sasa
Mathayo 1: NEN
Kuonyesha
Shirikisha
Nakili
Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia
Neno: Biblia Takatifu™ Neno™
Hakimiliki © 1984, 1989, 2009, 2015 na Biblica, Inc.
Imetumiwa kwa ruhusa. Haki zote zimehifadhiwa duniani kote.
Kiswahili Contemporary Version™
Copyright © 1984, 1989, 2009, 2015 by Biblica, Inc.
Used with Permission. All Rights Reserved Worldwide.