Mathayo 11:28-30
Mathayo 11:28-30 NENO
“Njooni kwangu, ninyi nyote mnaotaabika na kulemewa na mizigo, nami nitawapumzisha. Jifungeni nira yangu, mjifunze kutoka kwangu, kwa maana mimi ni mpole na mnyenyekevu wa moyo, nanyi mtapata raha katika nafsi zenu. Kwa maana nira yangu ni laini na mzigo wangu ni mwepesi.”