Mathayo 7:24-29
Mathayo 7:24-29 NENO
“Kwa hiyo kila mtu ayasikiaye haya maneno yangu na kuyatenda, ni kama mtu mwenye busara aliyejenga nyumba yake kwenye mwamba. Mvua ikanyesha, mafuriko yakaja, na upepo ukavuma ukaipiga hiyo nyumba. Lakini haikuanguka; kwa sababu msingi wake ulikuwa kwenye mwamba. Kila anayesikia haya maneno yangu na asiyatende ni kama mtu mjinga aliyejenga nyumba yake kwenye mchanga. Mvua ikanyesha, mafuriko yakaja, nao upepo ukavuma ukaipiga hiyo nyumba, nayo ikaanguka kwa kishindo kikubwa.” Isa alipomaliza kusema maneno haya, umati wa watu wakashangazwa sana na mafundisho yake, kwa sababu alifundisha kama yeye aliye na mamlaka, wala si kama walimu wao wa sheria.