Mathayo Utangulizi
Utangulizi
Mathayo alikuwa mtoza ushuru ambaye Bwana Isa alimwita awe mwanafunzi wake hapo mwanzoni mwa huduma yake ya hadharani. Mathayo alianza kueleza kwa kirefu kuhusu Isa alivyozaliwa na bikira Mariamu, alivyobatizwa, na kujaribiwa nyikani. Isa alihubiri kuhusu ufalme wa Mwenyezi Mungu, ambao ni wa kila mtu anayetaka kupata uzima wa milele. Mtu anaingia katika ufalme huu kwa kutubu dhambi na kumwamini Isa. Mathayo aliyagawa mafundisho ya Isa katika sehemu kuu tano: 1. Maadili, 2. Kueneza Injili, 3. Mifano, 4. Ushirika, na 5. Kuja kwa ufalme wa Mwenyezi Mungu. Sehemu ya mwisho ya Injili ya Mathayo inaeleza kuhusu kufa na kufufuka kwa Isa, na agizo alilolitoa kwa wote wanaomwamini kueneza Injili ulimwenguni kote.
Mwandishi
Mathayo aitwaye Lawi.
Kusudi
Kumtambulisha Isa kwa Wayahudi kuwa ndiye Masihi, na pia Mfalme wa milele.
Mahali
Palestina.
Tarehe
Mnamo 60–65 B.K.
Wahusika Wakuu
Isa na wanafunzi wake, Mariamu, Yahya na wanafunzi wake, viongozi wa dini ya Kiyahudi, na Pilato.
Wazo Kuu
Kuthibitisha kwamba Bwana Isa alikamilisha ahadi ambazo Mwenyezi Mungu alitoa katika Maandiko Matakatifu.
Mambo Muhimu
Kitabu hiki kinaelezea matukio manne ya maisha ya Isa ya utotoni. Pia kinaelezea mifano kumi aliyoitoa Isa, na miujiza miwili aliyoifanya. Ina midahalo tisa ambayo Isa alihojiana na baadhi ya watu. Kinamalizia na hisia sita zilizoandamana na kusulubiwa kwake, na maagizo kwa wanafunzi wake kueneza Injili duniani kote.
Yaliyomo
Maisha na huduma ya awali ya Isa (1:1–4:25)
Mahubiri ya Mlimani (5:1–7:29)
Mafundisho ya mifano na mazungumzo (8:1–18:35)
Safari ya kwenda Yerusalemu, na maonyo ya mwisho (19:1–23:39)
Unabii kuhusu mambo yajayo (24:1–25:46)
Kufa na kufufuka kwa Isa (26:1–28:20).
Iliyochaguliwa sasa
Mathayo Utangulizi: NENO
Kuonyesha
Shirikisha
Nakili
![None](/_next/image?url=https%3A%2F%2Fimageproxy.youversionapistaging.com%2F58%2Fhttps%3A%2F%2Fweb-assets.youversion.com%2Fapp-icons%2Fsw.png&w=128&q=75)
Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia
Neno: Maandiko Matakatifu™ NMM™
Hakimiliki © 2018, 2024 na Biblica, Inc.
Imetumiwa kwa ruhusa.
Haki zote zimehifadhiwa duniani kote.
Kiswahili Contemporary Scriptures™
Copyright © 2018, 2024 by Biblica, Inc.
Used with permission. All rights reserved worldwide.