Wafilipi Utangulizi
Utangulizi
Paulo alitembelea mji wa Filipi katika safari yake ya pili kueneza Injili, kutokana na maono aliyoyapata akiwa Troa kumwelezea aelekee Makedonia. Filipi hapakuwa na Sinagogi kwa sababu ya idadi ndogo ya Wayahudi. Waumini wa Filipi walimpelekea Paulo msaada kupitia kwa Epafrodito. Pia alitumia nafasi hiyo kuelezea matatizo aliyopata huko Rumi. Waumini wote waliambiwa wawe na malengo ya juu kabisa katika maisha yao ya wafuasi wa Al-Masihi, kwa maana Mwenyezi Mungu angewatimizia mahitaji yao yote katika maisha. Paulo aliwahimiza kufurahi nyakati zote.
Mwandishi
Mtume Paulo.
Kusudi
Kuwashukuru rafiki zake wapendwa waliokuwa wamempelekea msaada kwa ajili ya mahitaji yake. Kuwatia Wafilipi moyo na kuwataka kusimama imara, akiwahimiza wawe na unyenyekevu kama aliokuwa nao Al-Masihi, na pia wawe na umoja.
Mahali
Rumi.
Tarehe
Mnamo 61 B.K.
Wahusika Wakuu
Paulo, Timotheo, Epafrodito, Euodia na Sintike.
Wazo Kuu
Paulo alisisitiza kuhusu furaha ya muumini katika Al-Masihi.
Mambo Muhimu
Paulo anaagiza waumini kukataa kabisa mafundisho ya uongo na kuwahimiza wafurahi nyakati zote.
Yaliyomo
Paulo na matatizo yake huko Rumi (1:1-30)
Kumwiga Al-Masihi (2:1-30)
Mafundisho kuhusu mwenendo wa mfuasi wa Al-Masihi (3:1-21)
Mausia, shukrani na salamu za mwisho (4:1-23).
Iliyochaguliwa sasa
Wafilipi Utangulizi: NENO
Kuonyesha
Shirikisha
Nakili
Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia
Neno: Maandiko Matakatifu™ NMM™
Hakimiliki © 2018, 2024 na Biblica, Inc.
Imetumiwa kwa ruhusa.
Haki zote zimehifadhiwa duniani kote.
Kiswahili Contemporary Scriptures™
Copyright © 2018, 2024 by Biblica, Inc.
Used with permission. All rights reserved worldwide.