Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Mithali 24:13-22

Mithali 24:13-22 NEN

Ule asali mwanangu, kwa kuwa ni nzuri; asali kutoka kwenye sega ni tamu kwa kuonja. Ujue pia kwamba hekima ni tamu kwa nafsi yako, kama ukiipata, kuna matumaini kwako ya siku zijazo, nalo tumaini lako halitakatiliwa mbali. Usivizie kama haramia afanyavyo ili kuyashambulia makao ya mwenye haki, wala usiyavamie makazi yake, Kwa maana ingawa mtu mwenye haki huanguka mara saba, huinuka tena, lakini waovu huangushwa chini na maafa. Usitazame kwa kufurahia adui yako aangukapo; wakati ajikwaapo, usiruhusu moyo wako ushangilie. BWANA asije akaona na kuchukia akaiondoa ghadhabu yake mbali naye. Usikasirike kwa sababu ya watu wabaya wala usiwaonee wivu waovu, kwa maana mtu mbaya hana tumaini la siku zijazo, nayo taa ya waovu itazimwa. Mwanangu, mche BWANA na mfalme, wala usijiunge na waasi, kwa maana hao wawili watatuma maangamizi ya ghafula juu yao, naye ni nani ajuaye maafa wawezayo kuleta?