Methali 24:13-22
Methali 24:13-22 Biblia Habari Njema (BHN)
Mwanangu, ule asali maana ni nzuri; sega la asali ni tamu mdomoni. Ndivyo ilivyo hekima nafsini mwako; ukiipata utakuwa na matazamio mema, wala tumaini lako halitakuwa la bure. Usivizie kama mwovu kushambulia makao ya mtu mwema, wala usijaribu kuiharibu nyumba yake, maana mtu mwema huanguka mara nyingi lakini huinuka, lakini mtu mwovu huangamizwa na janga. Usishangilie kuanguka kwa adui yako; usifurahie moyoni mwako kujikwaa kwake, maana Mwenyezi-Mungu aonaye hayo hatapendezwa; huenda akaacha kumwadhibu. Usihangaike kwa sababu ya watenda mabaya, wala usiwaonee wivu watu waovu, maana mwovu hatakuwa na mema baadaye; taa ya uhai wake itazimwa. Mwanangu, umche Mwenyezi-Mungu na kumheshimu mfalme, wala usishirikiane na wale wasio na msimamo, maana maangamizi yao huwapata ghafla. Hakuna ajuaye maafa watakayozusha.
Methali 24:13-22 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Mwanangu, ule asali, kwa maana ni njema, Na sega la asali lililo tamu ulionjapo. Basi utaijua hekima kuwa tamu kwa nafsi yako; Ikiwa umekwisha kuiona; Ndipo itakapofuata thawabu; Wala tumaini lako halitabatilika. Ewe mtu mbaya, usiyavizie makao yake mwenye haki; Wala usipaharibu mahali pake pa kupumzika; Kwa maana mwenye haki huanguka mara saba akaondoka tena; Bali wasio haki hukwazwa na mabaya. Usifurahi, adui yako aangukapo; Wala moyo wako usishangilie ajikwaapo; BWANA asije akaliona hilo, likamkasirisha; Akageuzia mbali naye hasira yake. Usikasirike kwa sababu ya watenda mabaya; Wala usiwahusudu wabaya; Kwa maana mtu mbaya hapati thawabu; Taa ya mtu mbaya itazimika. Mwanangu, mche BWANA, na mfalme; Wala usishirikiane na wenye kigeugeu; Maana msiba wao utatokea kwa ghafla; Tena ni nani aujuaye uharibifu wa miaka yao.
Methali 24:13-22 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Mwanangu, ule asali, kwa maana ni njema, Na sega la asali lililo tamu ulionjapo. Basi utaijua hekima kuwa tamu kwa nafsi yako; Ikiwa umekwisha kuiona; Ndipo itakapofuata thawabu; Wala tumaini lako halitabatilika. Ewe mtu mbaya, usiyavizie makao yake mwenye haki; Wala usipaharibu mahali pake pa kupumzika; Kwa maana mwenye haki huanguka mara saba akaondoka tena; Bali wasio haki hukwazwa na mabaya. Usifurahi, adui yako aangukapo; Wala moyo wako usishangilie ajikwaapo; BWANA asije akaliona hilo, likamkasirisha; Akageuzia mbali naye hasira yake. Usikasirike kwa sababu ya watenda mabaya; Wala usiwahusudu wabaya; Kwa maana mtu mbaya hapati thawabu; Taa ya mtu mbaya itazimika. Mwanangu, mche BWANA, na mfalme; Wala usishirikiane na wenye kigeugeu; Maana msiba wao utatokea kwa ghafula; Tena ni nani aujuaye uharibifu wa miaka yao.
Methali 24:13-22 Neno: Bibilia Takatifu (NEN)
Ule asali mwanangu, kwa kuwa ni nzuri; asali kutoka kwenye sega ni tamu kwa kuonja. Ujue pia kwamba hekima ni tamu kwa nafsi yako, kama ukiipata, kuna matumaini kwako ya siku zijazo, nalo tumaini lako halitakatiliwa mbali. Usivizie kama haramia afanyavyo ili kuyashambulia makao ya mwenye haki, wala usiyavamie makazi yake, Kwa maana ingawa mtu mwenye haki huanguka mara saba, huinuka tena, lakini waovu huangushwa chini na maafa. Usitazame kwa kufurahia adui yako aangukapo; wakati ajikwaapo, usiruhusu moyo wako ushangilie. BWANA asije akaona na kuchukia akaiondoa ghadhabu yake mbali naye. Usikasirike kwa sababu ya watu wabaya wala usiwaonee wivu waovu, kwa maana mtu mbaya hana tumaini la siku zijazo, nayo taa ya waovu itazimwa. Mwanangu, mche BWANA na mfalme, wala usijiunge na waasi, kwa maana hao wawili watatuma maangamizi ya ghafula juu yao, naye ni nani ajuaye maafa wawezayo kuleta?