Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Mit 24

24
1Usiwahusudu watu waovu,
Wala usitamani kuwa pamoja nao;
2Kwa maana moyo wao hufikiri dhuluma,
Na midomo yao huongea madhara.
3Nyumba hujengwa kwa hekima,
Na kwa ufahamu huthibitika,
4Na kwa maarifa vyumba vyake hujazwa
Vitu vyote vya thamani na vya kupendeza.
5Mtu mwenye hekima ana nguvu;
Naam, mtu wa maarifa huongeza uwezo;
6Maana kwa mashauri ya akili utafanya vita;
Na kwa wingi wa washauri huja wokovu.
7Kwa mpumbavu hekima haipatikani;
Hafumbui kinywa chake langoni.
8Mtu afikiriye kutenda maovu,
Watu watamwita mtundu;
9 # Mwa 6:5; Zab 119:113; Mt 9:4; Mdo 8:22; 2 Kor 10:5 Fikira za mpumbavu ni dhambi,
Na mwenye mzaha huwachukiza watu.
10Ukizimia siku ya taabu,
Nguvu zako ni chache.
11 # Isa 58:6,7; 1 Yoh 3:16 Uwaokoe wanaochukuliwa ili wauawe;
Nao walio tayari kuchinjwa uwaopoe.
12 # Ayu 34:11; Yer 32:19; Rum 2:6; Ufu 2:23 Ukisema, Sisi hatukujua hayo;
Je! Yeye aipimaye mioyo siye afahamuye?
Naye ailindaye nafsi yako siye ajuaye?
Je! Hatamlipa kila mtu sawasawa na kazi yake?
13Mwanangu, ule asali, kwa maana ni njema,
Na sega la asali lililo tamu ulionjapo.
14Basi utaijua hekima kuwa tamu kwa nafsi yako;
Ikiwa umekwisha kuiona;
Ndipo itakapofuata thawabu;
Wala tumaini lako halitabatilika.
15Ewe mtu mbaya, usiyavizie makao yake mwenye haki;
Wala usipaharibu mahali pake pa kupumzika;
16 # Zab 34:19; Mik 7:8 Kwa maana mwenye haki huanguka mara saba akaondoka tena;
Bali wasio haki hukwazwa na mabaya.
17Usifurahi, adui yako aangukapo;
Wala moyo wako usishangilie ajikwaapo;
18BWANA asije akaliona hilo, likamkasirisha;
Akageuzia mbali naye hasira yake.
19Usikasirike kwa sababu ya watenda mabaya;
Wala usiwahusudu wabaya;
20 # Zab 11:6; Isa 3:11 Kwa maana mtu mbaya hapati thawabu;
Taa ya mtu mbaya itazimika.
21 # Rum 13:7; 1 Pet 2:17 Mwanangu, mche BWANA, na mfalme;
Wala usishirikiane na wenye kigeugeu;
22Maana msiba wao utatokea kwa ghafula;
Tena ni nani aujuaye uharibifu wa miaka yao.
Maneno Mengine ya Wenye Hekima
23 # Kum 1:17; 2 Nya 19:7; Mit 18:5; Yn 7:24 Haya nayo pia ni maneno ya wenye akili.
Kupendelea watu katika hukumu si kwema.
24 # Isa 5:23 Amwambiaye mtu mwovu, Wewe una haki;
Kabila za watu watamlaani, taifa watamchukia.
25Bali kwao wakemeao furaha itakuwako;
Na baraka ya kufanikiwa itawajilia.
26Aibusu midomo atoaye jawabu la haki.
27Tengeneza kazi yako huko nje,
Jifanyizie kazi yako tayari shambani,
Ukiisha, jenga nyumba yako.
28 # Efe 4:25 Usimshuhudie jirani yako pasipo sababu,
Wala usidanganye kwa midomo yako.
29 # Mt 5:39 Usiseme, Nitamtenda kama alivyonitenda mimi;
Nitamlipa mtu huyo sawasawa na tendo lake.
30Nalipita karibu na shamba la mvivu,
Na shamba la mizabibu la mtu asiye na akili.
31 # Yer 4:3; Mt 13:7,22; Ebr 6:8 Kumbe! Lote pia limemea miiba;
Uso wake ulifunikwa kwa viwawi;
Na ukuta wake wa mawe umebomoka.
32Ndipo nilipoangalia na kufikiri sana;
Naliona, nikapata mafundisho.
33 # Mit 6:10-11 Bado kulala kidogo, kusinzia kidogo,
Bado kukunja mikono upate usingizi!
34Hivyo, umaskini wako huja kama mnyang’anyi,
Na uhitaji wako kama mtu mwenye silaha.
KITABU CHA NNE

Iliyochaguliwa sasa

Mit 24: SUV

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia