Mit 23
23
1Utakapoketi kwa chakula pamoja na mtawala,
Mwangalie sana yeye aliye mbele yako.
2Tena ujitie kisu kooni,
Kama ukiwa mlafi.
3Usivitamani vyakula vyake vya anasa;
Kwa maana ni vyakula vya hila.
4 #
Mit 28:20; 3:5; Yn 6:27; 1 Tim 6:9; Rum 12:16 Usijitaabishe ili kupata utajiri;
Acha kuzitegemea akili zako mwenyewe.
5Je! Utavikazia macho vile ambavyo si kitu?
Maana bila shaka mali hujifanyia mabawa,
Kama tai arukaye mbinguni.
6 #
Zab 141:4; Kum 15:9; Mt 20:15; Mk 7:22 Usile mkate wa mtu mwenye husuda;
Wala usivitamani vyakula vyake vya anasa;
7Maana aonavyo nafsini mwake, ndivyo alivyo.
Akuambia, Haya, kula, kunywa;
Lakini moyo wake hauwi pamoja nawe.
8Tonge lile ulilokula utalitapika,
Na maneno yako matamu yatakupotea.
9 #
Mt 7:6
Usiseme masikioni mwa mpumbavu;
Maana atadharau hekima ya maneno yako.
10Usiiondoe alama ya mpaka wa zamani;
Wala usiingie katika mashamba ya yatima;
11 #
Ayu 31:21; Yer 50:34 Kwa sababu mkombozi wao ana nguvu;
Atawatetea juu yako.
12Elekeza moyo wako kusikiliza mafundisho;
Tega masikio yako kusikia maneno ya maarifa.
13Usimnyime mtoto wako mapigo;
Maana ukimpiga kwa fimbo hatakufa.
14 #
1 Kor 5:5
Utampiga kwa fimbo,
Na kumwokoa nafsi yake na Kuzimu.
15Mwanangu, kama moyo wako una hekima,
Moyo wangu utafurahi, naam, moyo wangu;
16Naam, viuno vyangu vitafurahi,
Midomo yako inenapo maneno mema.
17Moyo wako usiwahusudu wenye dhambi;
Bali mche BWANA mchana kutwa;
18 #
Lk 16:25
Maana bila shaka iko thawabu;
Na tumaini lako halitabatilika.
19Sikia, mwanangu, uwe na hekima,
Na kuuongoza moyo wako katika njia njema.
20 #
Isa 5:22; Mt 24:49; Lk 21:34; Rum 13:13; Efe 5:18 Usiwe miongoni mwao wanywao mvinyo;
Miongoni mwao walao nyama kwa pupa.
21Kwa maana mlevi na mlafi huingia umaskini,
Na utepetevu humvika mtu nguo mbovu.
22 #
Efe 6:1
Msikilize baba yako aliyekuzaa,
Wala usimdharau mama yako akiwa mzee.
23 #
Mt 13:44
Inunue kweli, wala usiiuze;
Naam, hekima, na mafundisho, na ufahamu.
24Baba yake mwenye haki atashangilia;
Naye amzaaye mtoto mwenye hekima atamfurahia.
25Na wafurahi baba yako na mama yako;
Na afurahi aliyekuzaa.
26Mwanangu, nipe moyo wako;
Macho yako yapendezwe na njia zangu.
27Kwa maana kahaba ni shimo refu;
Na malaya ni rima jembamba.
28Naam, huotea kama mnyang’anyi;
Huwaongeza wenye hila katika wanadamu.
29 #
1 Fal 20:16; Mit 20:1; Isa 5:11; Nah 1:10; Mt 24:49,50; Efe 5:18 Ni nani apigaye, Yowe? Ni nani aliaye, Ole?
Ni nani mwenye ugomvi? Ni nani mwenye mguno?
Ni nani aliye na jeraha zisizo na sababu?
Ni nani aliye na macho mekundu?
30Ni wale wakaao sana kwenye mvinyo;
Waendao kutafuta divai iliyochanganyika.
31Usiitazame mvinyo iwapo ni nyekundu;
Iitiapo bilauri rangi yake, ishukapo taratibu;
32Mwisho wake huuma kama nyoka;
Huchoma kama fira.
33Macho yako yataona mambo mageni;
Na moyo wako utatoa yaliyopotoka.
34Naam, utakuwa kama alalaye katikati ya bahari;
Au kama yeye asinziaye juu ya mlingoti.
35 #
Mit 27:22; Yer 5:3; Kum 29:19; Isa 56:12; 2 Pet 2:22 Utasema, Wamenichapa wala sikuumia;
Wamenipiga wala sina habari;
Nitaamka lini, nitazidi kuitafuta tena.
Iliyochaguliwa sasa
Mit 23: SUV
Kuonyesha
Shirikisha
Nakili
Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia
Swahili Union Version (SUV): © Bible Society of Tanzania and Bible Society of Kenya, 1952, 1997. All rights reserved. lt/pgt ltpgtSwahili Union Version (SUV): Hakimiliki -1952, 1997: kwa: Chama cha Biblia cha Tanzania na Chama cha Biblia cha Kenya. Haki zote zimehifadhiwa.