Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Mithali 27

27
1Usijisifu kwa ajili ya kesho,
kwa kuwa hujui ni nini kitakachozaliwa kwa siku moja.
2Mwache mwingine akusifu,
wala si kinywa chako mwenyewe;
mtu mwingine afanye hivyo
na si midomo yako mwenyewe.
3Jiwe ni zito na mchanga ni mzigo,
lakini kukasirishwa na mpumbavu ni kuzito kuliko vyote viwili.
4Hasira ni ukatili na ghadhabu kali ni gharika,
lakini ni nani awezaye kusimama mbele ya wivu?
5Afadhali karipio la wazi
kuliko upendo uliofichika.
6Majeraha kutoka kwa rafiki yaonesha uaminifu,
lakini adui huzidisha busu.
7Yeye aliyeshiba huchukia kabisa asali,
bali kwa mwenye njaa
hata kile kilicho kichungu
kwake ni kitamu.
8Kama ndege atangatangavyo mbali na kiota chake,
ndivyo alivyo mtu atangatangaye
mbali na nyumbani mwake.
9Manukato na uvumba huleta furaha moyoni,
nao uzuri wa rafiki huchipuka
katika ushauri wake wa uaminifu.
10Usimwache rafiki yako wala rafiki wa baba yako,
tena usiende nyumbani mwa ndugu yako
wakati umepatwa na maafa.
Bora jirani wa karibu
kuliko ndugu aliye mbali.
11Mwanangu, uwe na hekima,
nawe ulete furaha moyoni mwangu,
ndipo nitakapoweza kumjibu yeyote
anitendaye kwa dharau.
12Mtu mwenye busara huona hatari na kujificha,
bali mjinga huendelea mbele, naye hupata madhara.
13Chukua vazi la yule awekaye dhamana
kwa ajili ya mgeni;
lishikilie liwe dhamana
kwa ajili ya mgeni.
14Mtu akimbariki jirani yake kwa sauti kuu
asubuhi na mapema,
itahesabiwa kuwa ni laana.
15Mke mgomvi ni kama
matone yasiyokoma siku ya mvua.
16Kumzuia ni kama kuuzuia upepo,
au kukamata mafuta kwa kiganja cha mkono.
17Kama vile chuma kinoavyo chuma,
ndivyo mtu amnoavyo mwenzake.
18Yeye autunzaye mtini atakula tunda lake,
naye amtunzaye bwana wake ataheshimiwa.
19Kama uso uonekanavyo kwenye maji,
ndivyo hivyo moyo wa mtu humwonesha alivyo.
20Kuzimu#27:20 Kuzimu kwa Kiebrania ni Sheol, yaani Shimo lisilo na mwisho. na Uharibifu#27:20 kwa Kiebrania ni Abadon havishibi,
wala macho ya mwanadamu hayashibi.
21Kalibu husafisha fedha na tanuru husafisha dhahabu,
bali mtu hupimwa kwa sifa anazopewa na watu.
22Hata ukimtwanga mpumbavu kwenye kinu,
ukimtwanga kama nafaka kwa mchi,
hutauondoa upumbavu wake.
23Hakikisha kuwa unajua hali ya makundi yako ya kondoo na mbuzi;
angalia ng’ombe wako kwa makini.
24Kwa kuwa utajiri haudumu milele,
nalo taji halidumu vizazi vyote.
25Wakati majani makavu yameondolewa
na mapya yamechipua,
nayo majani toka milimani yamekusanywa,
26wana-kondoo watakupatia mavazi
na mbuzi thamani ya shamba.
27Utakuwa na maziwa mengi ya mbuzi
kukulisha wewe na jamaa yako,
na kuwalisha wajakazi wako.

Iliyochaguliwa sasa

Mithali 27: NENO

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia