Zaburi 130:1-8
Zaburi 130:1-8 NEN
Kutoka vilindini ninakulilia, Ee BWANA. Ee BWANA, sikia sauti yangu. Masikio yako na yawe masikivu kwa kilio changu unihurumie. Kama wewe, Ee BWANA, ungeweka kumbukumbu ya dhambi, Ee Bwana, ni nani angeliweza kusimama? Lakini kwako kuna msamaha, kwa hiyo wewe unaogopwa. Namngojea BWANA, nafsi yangu inangojea, katika neno lake naweka tumaini langu. Nafsi yangu inamngojea Bwana kuliko walinzi waingojeavyo asubuhi, naam, kuliko walinzi waingojeavyo asubuhi. Ee Israeli, mtumaini BWANA, maana kwa BWANA kuna upendo usiokoma, na kwake kuna ukombozi kamili. Yeye mwenyewe ataikomboa Israeli kutoka dhambi zao zote.