Zab 130:1-8
Zab 130:1-8 SUV
Ee BWANA, toka vilindini nimekulilia. Bwana, uisikie sauti yangu. Masikio yako na yaisikilize Sauti ya dua zangu. BWANA, kama Wewe ungehesabu maovu, Ee Bwana, nani angesimama? Lakini kwako kuna msamaha, Ili Wewe uogopwe. Nimemngoja BWANA, roho yangu imengoja, Na neno lake nimelitumainia. Nafsi yangu inamngoja Bwana, Kuliko walinzi waingojavyo asubuhi, Naam, walinzi waingojao asubuhi. Ee Israeli, umtarajie BWANA; Maana kwa BWANA kuna fadhili, Na kwake kuna ukombozi mwingi. Yeye atamkomboa Israeli na maovu yake yote.