Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Zab 130

130
Kusubiri Wokovu wa Mungu
Wimbo wa kupanda mlima.
1 # Omb 3:55; Yon 2:2 Ee BWANA, toka vilindini nimekulilia.
2Bwana, uisikie sauti yangu.
Masikio yako na yaisikilize
Sauti ya dua zangu.
3 # Zab 143:2; Yn 8:7-9; Rum 3:20 BWANA, kama Wewe ungehesabu maovu,
Ee Bwana, nani angesimama?
4 # 2 The 1:6; Zab 37:2; Yer 17:6; Kut 3:4,7; Efe 1:7; 1 Fal 8:40; Yer 33:8,9; Ebr 12:28 Lakini kwako kuna msamaha,
Ili Wewe uogopwe.
5 # Isa 26:8 Nimemngoja BWANA, roho yangu imengoja,
Na neno lake nimelitumainia.
6Nafsi yangu inamngoja Bwana,
Kuliko walinzi waingojavyo asubuhi,
Naam, walinzi waingojao asubuhi.
7 # Isa 55:7 Ee Israeli, umtarajie BWANA;
Maana kwa BWANA kuna fadhili,
Na kwake kuna ukombozi mwingi.
8 # Mt 1:21; Tit 2:14 Yeye atamkomboa Israeli na maovu yake yote.

Iliyochaguliwa sasa

Zab 130: SUV

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia