Zaburi 136:1-12
Zaburi 136:1-12 NEN
Mshukuruni BWANA, kwa kuwa ni mwema. Fadhili zake zadumu milele. Mshukuruni Mungu wa miungu. Fadhili zake zadumu milele. Mshukuruni Bwana wa mabwana: Fadhili zake zadumu milele. Kwake yeye pekee atendaye maajabu makuu, Fadhili zake zadumu milele. Ambaye kwa ufahamu wake aliziumba mbingu, Fadhili zake zadumu milele. Ambaye aliitandaza dunia juu ya maji, Fadhili zake zadumu milele. Ambaye aliumba mianga mikubwa, Fadhili zake zadumu milele. Jua litawale mchana, Fadhili zake zadumu milele. Mwezi na nyota vitawale usiku, Fadhili zake zadumu milele. Kwake yeye aliyemuua mzaliwa wa kwanza wa Misri, Fadhili zake zadumu milele. Na kuwatoa Israeli katikati yao, Fadhili zake zadumu milele. Kwa mkono wenye nguvu ulionyooshwa, Fadhili zake zadumu milele.