Zaburi 136:1-12
Zaburi 136:1-12 Biblia Habari Njema (BHN)
Mshukuruni Mwenyezi-Mungu kwa kuwa ni mwema; kwa maana fadhili zake zadumu milele. Mshukuruni Mungu wa miungu; kwa maana fadhili zake zadumu milele. Mshukuruni Bwana wa mabwana; kwa maana fadhili zake zadumu milele. Ndiye peke yake atendaye makuu ya ajabu; kwa maana fadhili zake zadumu milele. Ndiye aliyeziumba mbingu kwa hekima; kwa maana fadhili zake zadumu milele. Ndiye aliyeitengeneza nchi juu ya vilindi vya maji; kwa maana fadhili zake zadumu milele. Ndiye aliyeumba jua, mwezi na nyota; kwa maana fadhili zake zadumu milele. Jua liutawale mchana; kwa maana fadhili zake zadumu milele. Mwezi na nyota vitawale usiku; kwa maana fadhili zake zadumu milele. Ndiye aliyewaua wazaliwa wa kwanza wa Misri; kwa maana fadhili zake zadumu milele. Akawaondoa watu wa Israeli kutoka huko; kwa maana fadhili zake zadumu milele. Kwa mkono wake wenye nguvu na enzi; kwa maana fadhili zake zadumu milele.
Zaburi 136:1-12 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Mshukuruni BWANA kwa kuwa ni mwema; Kwa maana fadhili zake ni za milele. Mshukuruni Mungu wa miungu; Kwa maana fadhili zake ni za milele. Mshukuruni Bwana wa mabwana; Kwa maana fadhili zake ni za milele. Yeye peke yake afanya maajabu makuu; Kwa maana fadhili zake ni za milele. Yeye aliyeumba mbingu kwa fahamu zake; Kwa maana fadhili zake ni za milele. Yeye aliyeitandaza nchi juu ya maji; Kwa maana fadhili zake ni za milele. Yeye aliyeumba mianga mikubwa; Kwa maana fadhili zake ni za milele. Jua litawale mchana; Kwa maana fadhili zake ni za milele. Mwezi na nyota zitawale usiku; Kwa maana fadhili zake ni za milele. Yeye aliyewapiga Wamisri kwa kuwaua wazaliwa wao wa kwanza; Kwa maana fadhili zake ni za milele. Akawatoa Waisraeli katikati yao; Kwa maana fadhili zake ni za milele. Kwa mkono hodari na mkono ulionyoshwa; Kwa maana fadhili zake ni za milele.
Zaburi 136:1-12 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Mshukuruni BWANA kwa kuwa ni mwema; Kwa maana fadhili zake ni za milele. Mshukuruni Mungu wa miungu; Kwa maana fadhili zake ni za milele. Mshukuruni Bwana wa mabwana; Kwa maana fadhili zake ni za milele. Yeye peke yake afanya maajabu makuu; Kwa maana fadhili zake ni za milele. Yeye aliyefanya mbingu kwa fahamu zake; Kwa maana fadhili zake ni za milele. Yeye aliyeitandaza nchi juu ya maji; Kwa maana fadhili zake ni za milele. Yeye aliyefanya mianga mikubwa; Kwa maana fadhili zake ni za milele. Jua litawale mchana; Kwa maana fadhili zake ni za milele. Mwezi na nyota zitawale usiku; Kwa maana fadhili zake ni za milele. Yeye aliyewapiga Wamisri kwa kuwaua wazaliwa wa kwanza wao; Kwa maana fadhili zake ni za milele. Akawatoa Waisraeli katikati yao; Kwa maana fadhili zake ni za milele. Kwa mkono hodari na mkono ulionyoshwa; Kwa maana fadhili zake ni za milele.
Zaburi 136:1-12 Neno: Bibilia Takatifu (NEN)
Mshukuruni BWANA, kwa kuwa ni mwema. Fadhili zake zadumu milele. Mshukuruni Mungu wa miungu. Fadhili zake zadumu milele. Mshukuruni Bwana wa mabwana: Fadhili zake zadumu milele. Kwake yeye pekee atendaye maajabu makuu, Fadhili zake zadumu milele. Ambaye kwa ufahamu wake aliziumba mbingu, Fadhili zake zadumu milele. Ambaye aliitandaza dunia juu ya maji, Fadhili zake zadumu milele. Ambaye aliumba mianga mikubwa, Fadhili zake zadumu milele. Jua litawale mchana, Fadhili zake zadumu milele. Mwezi na nyota vitawale usiku, Fadhili zake zadumu milele. Kwake yeye aliyemuua mzaliwa wa kwanza wa Misri, Fadhili zake zadumu milele. Na kuwatoa Israeli katikati yao, Fadhili zake zadumu milele. Kwa mkono wenye nguvu ulionyooshwa, Fadhili zake zadumu milele.