Zaburi 136:1-12
Zaburi 136:1-12 BHN
Mshukuruni Mwenyezi-Mungu kwa kuwa ni mwema; kwa maana fadhili zake zadumu milele. Mshukuruni Mungu wa miungu; kwa maana fadhili zake zadumu milele. Mshukuruni Bwana wa mabwana; kwa maana fadhili zake zadumu milele. Ndiye peke yake atendaye makuu ya ajabu; kwa maana fadhili zake zadumu milele. Ndiye aliyeziumba mbingu kwa hekima; kwa maana fadhili zake zadumu milele. Ndiye aliyeitengeneza nchi juu ya vilindi vya maji; kwa maana fadhili zake zadumu milele. Ndiye aliyeumba jua, mwezi na nyota; kwa maana fadhili zake zadumu milele. Jua liutawale mchana; kwa maana fadhili zake zadumu milele. Mwezi na nyota vitawale usiku; kwa maana fadhili zake zadumu milele. Ndiye aliyewaua wazaliwa wa kwanza wa Misri; kwa maana fadhili zake zadumu milele. Akawaondoa watu wa Israeli kutoka huko; kwa maana fadhili zake zadumu milele. Kwa mkono wake wenye nguvu na enzi; kwa maana fadhili zake zadumu milele.