Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Zaburi 138

138
Zaburi 138
Maombi ya shukrani
Zaburi ya Daudi.
1Nitakusifu wewe, Ee Mwenyezi Mungu, kwa moyo wangu wote,
mbele ya “miungu” nitaimba sifa zako.
2Nitasujudu nikielekea Hekalu lako takatifu,
nami nitalisifu jina lako
kwa ajili ya upendo wako
na uaminifu,
kwa maana umeitukuza ahadi yako
zaidi ya jina lako.
3Nilipoita, ulinijibu;
ulinifanya jasiri na mwenye moyo hodari.
4Wafalme wote wa dunia wakusifu wewe Ee Mwenyezi Mungu,
wakati wanaposikia maneno ya kinywa chako.
5Wao na waimbe kuhusu njia za Mwenyezi Mungu,
kwa maana utukufu wa Mwenyezi Mungu ni mkuu.
6Ingawa Mwenyezi Mungu yuko juu,
humwangalia mnyonge,
bali mwenye kiburi
yeye anamjua kutokea mbali.
7Nijapopita katikati ya shida,
wewe unayahifadhi maisha yangu,
unanyoosha mkono wako dhidi ya hasira ya adui zangu,
kwa mkono wako wa kuume unaniokoa.
8Mwenyezi Mungu atatimiza kusudi lake kwangu,
Ee Mwenyezi Mungu, upendo wako wadumu milele:
usiziache kazi za mikono yako.

Iliyochaguliwa sasa

Zaburi 138: NENO

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia