Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Zaburi 24

24
Zaburi 24
Mfalme mkuu
Zaburi ya Daudi.
1Dunia ni mali ya Mwenyezi Mungu, na vyote vilivyomo,
ulimwengu, na wote wanaoishi ndani yake,
2maana aliiwekea misingi yake baharini,
na kuifanya imara juu ya maji.
3Nani awezaye kuupanda mlima wa Mwenyezi Mungu?
Ni nani awezaye kusimama patakatifu pake?
4Ni yule mwenye mikono safi na moyo mweupe,
yule ambaye hakuinulia sanamu nafsi yake
au kuapa kwa kitu cha uongo.
5Huyo atapokea baraka kutoka kwa Mwenyezi Mungu,
na hukumu ya haki kutoka kwa Mungu Mwokozi wake.
6Hiki ndicho kizazi cha wale wanaomtafuta,
wale wanaoutafuta uso wako, Ee Mungu wa Yakobo.
7Inueni vichwa vyenu, enyi malango,
inukeni enyi milango ya kale,
ili mfalme wa utukufu apate kuingia.
8Ni nani huyu Mfalme wa utukufu?
Ni Mwenyezi Mungu aliye na nguvu na uweza,
ni Mwenyezi Mungu aliye hodari katika vita.
9Inueni vichwa vyenu, enyi malango,
viinueni juu enyi milango ya kale,
ili Mfalme wa utukufu apate kuingia.
10Ni nani yeye, huyu Mfalme wa utukufu?
Ni Mwenyezi Mungu,
Mungu wa majeshi ya mbinguni;
yeye ndiye Mfalme wa utukufu.

Iliyochaguliwa sasa

Zaburi 24: NENO

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia