Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Zaburi 3:1-6

Zaburi 3:1-6 NENO

Ee Mwenyezi Mungu, tazama adui zangu walivyo wengi! Ni wengi kiasi gani wanaoinuka dhidi yangu! Wengi wanasema juu yangu, “Mungu hatamwokoa.” Lakini wewe, Ee Mwenyezi Mungu, ni ngao yangu pande zote; umeniwekea utukufu na kuinua kichwa changu. Ninamlilia Mwenyezi Mungu kwa sauti kuu, naye ananijibu kutoka mlima wake mtakatifu. Ninajilaza na kupata usingizi; naamka tena, kwa maana Mwenyezi Mungu hunitegemeza. Sitaogopa makumi elfu ya adui, wanaojipanga dhidi yangu kila upande.