Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Zaburi 3

3
Zaburi 3
Sala ya asubuhi ya kuomba msaada
Zaburi ya Daudi. Alipomkimbia mwanawe Absalomu.
1Ee Mwenyezi Mungu, tazama adui zangu walivyo wengi!
Ni wengi kiasi gani wanaoinuka dhidi yangu!
2Wengi wanasema juu yangu,
“Mungu hatamwokoa.”
3Lakini wewe, Ee Mwenyezi Mungu, ni ngao yangu pande zote;
umeniwekea utukufu na kuinua kichwa changu.
4Ninamlilia Mwenyezi Mungu kwa sauti kuu,
naye ananijibu kutoka mlima wake mtakatifu.
5Ninajilaza na kupata usingizi;
naamka tena, kwa maana Mwenyezi Mungu hunitegemeza.
6Sitaogopa makumi elfu ya adui,
wanaojipanga dhidi yangu kila upande.
7Ee Mwenyezi Mungu, amka!
Niokoe, Ee Mungu wangu!
Wapige adui zangu wote kwenye taya,
vunja meno ya waovu.
8Kwa maana wokovu watoka kwa Mwenyezi Mungu.
Baraka yako na iwe juu ya watu wako.

Iliyochaguliwa sasa

Zaburi 3: NENO

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia