Zaburi 34:3-5
Zaburi 34:3-5 NENO
Mtukuzeni Mwenyezi Mungu pamoja nami, naam, na tulitukuze jina lake pamoja. Nilimtafuta Mwenyezi Mungu naye akanijibu, akaniokoa kwenye hofu zangu zote. Wale wamtazamao hutiwa nuru, nyuso zao hazifunikwi na aibu kamwe.