Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Zaburi 36:5-10

Zaburi 36:5-10 NENO

Upendo wako, Ee Mwenyezi Mungu, unafika hadi mbinguni, uaminifu wako hadi kwenye anga. Haki yako ni kama milima mikubwa, hukumu zako ni kama kilindi kikuu. Ee Mwenyezi Mungu, wewe huwahifadhi mwanadamu na mnyama. Upendo wako usiokoma ni wa thamani mno! Watu wakuu na wadogo hujificha uvulini wa mabawa yako. Wanajifurahisha katika wingi ulio nyumbani mwako, nawe utawanywesha katika mto wa furaha zako. Kuwa pamoja nawe ni kijito cha uzima, katika nuru yako twaona nuru. Dumisha upendo wako kwa wale wanaokujua wewe, haki yako kwa wale walio wanyofu wa moyo.