Zaburi 69:13-18
Zaburi 69:13-18 NENO
Lakini Ee Mwenyezi Mungu, ninakuomba, kwa wakati ukupendezao; katika upendo wako mkuu, Ee Mungu, unijibu kwa wokovu wako wa hakika. Uniokoe katika matope, usiniache nizame; niokoe na hao wanaonichukia, kutoka kwa vilindi vya maji. Usiache mafuriko yanigharikishe au vilindi vinimeze, au shimo lifumbe kinywa chake juu yangu. Ee Mwenyezi Mungu, unijibu, kwa wema wa upendo wako; kwa huruma zako nyingi unigeukie. Usimfiche mtumishi wako uso wako, uharakishe kunijibu, kwa sababu niko katika shida. Njoo karibu uniokoe, nikomboe kwa sababu ya adui zangu.