Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Zaburi 97

97
Zaburi 97
Mwenyezi Mungu Mtawala mkuu
1Mwenyezi Mungu anatawala, nchi na ifurahi,
visiwa vyote vishangilie.
2Mawingu na giza nene vinamzunguka,
haki na hukumu ndio msingi wa kiti chake cha enzi.
3Moto hutangulia mbele zake
na huteketeza adui zake pande zote.
4Umeme wake wa radi humulika dunia,
nchi huona na kutetemeka.
5Milima huyeyuka kama nta mbele za Mwenyezi Mungu,
mbele za Bwana wa dunia yote.
6Mbingu zinatangaza haki yake,
na mataifa yote huona utukufu wake.
7Wote waabuduo sanamu waaibishwa,
wale wajisifiao sanamu:
mwabuduni yeye, enyi miungu yote!
8Sayuni husikia na kushangilia,
vijiji vya Yuda vinafurahi
kwa sababu ya hukumu zako, Ee Mwenyezi Mungu.
9Kwa kuwa wewe, Ee Mwenyezi Mungu, ndiwe Uliye Juu Sana kuliko dunia yote;
umetukuka sana juu ya miungu yote.
10Wale wanaompenda Mwenyezi Mungu na wauchukie uovu,
kwa maana yeye hulinda maisha ya waaminifu wake
na kuwaokoa kutoka mkononi mwa mwovu.
11Nuru huangaza wenye haki
na furaha kwa watu wanyofu wa moyo.
12Furahini katika Mwenyezi Mungu, enyi wenye haki,
lisifuni jina lake takatifu.

Iliyochaguliwa sasa

Zaburi 97: NENO

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia